You can edit almost every page by Creating an account and confirming your email.

Dr. Annie Msuya Lasway

From EverybodyWiki Bios & Wiki

File:Dr. Annie.jpg
Dr. Annie Msuya Lasway
BornEnikunda Amanda Kokiambo Benjamin Msuya
Songea, Tanzania
🏳️ NationalityTanzanian
🏫 EducationGeorge Mason University (BSc, MPH, PhD)
💼 Occupation
Health information specialist, researcher, and autism advocate
Known forFounding DECODER Health, advocating for autism spectrum disorder (ASD) awareness

Dr. Annie Msuya Lasway (jina la kuzaliwa: Enikunda Amanda Kokiambo Benjamin Msuya) ni mtaalamu wa taarifa za afya, mtafiti na mshauri wa haki za watu wenye Usonji (Autism Spectrum Disorder - ASD) kutoka Tanzania. Yeye ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa DECODER Health, shirika linalojihusisha na utafiti, huduma za afya ya tabia, na utetezi kwa ajili ya watu wenye usonji.

Maisha ya awali na elimu

Dr. Lasway alizaliwa katika Hospitali ya Peramiho, mjini Songea, Tanzania. Alianza elimu yake jijini London, Uingereza, wakati baba yake, Marehemu Meja Jenerali Benjamin Msuya, alipokuwa mjumbe wa kijeshi. Baadaye alihamia Tanzania na kuhudhuria Shule ya Msingi ya Bunge na Shule ya Sekondari ya Jangwani.

Alipata Shahada ya Kwanza ya Sayansi (BSc), Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma (MPH), na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Taarifa za Afya kutoka George Mason University nchini Marekani.[1]

Kazi na mchango wa kijamii

Kupitia shirika la DECODER Health, Dr. Lasway amekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kuhusu usonji na kupunguza unyanyapaa unaowakumba watu wenye hali hiyo. Shirika lake hushirikiana na taasisi mbalimbali katika kutoa huduma na elimu ya afya ya tabia, ikiwa ni pamoja na:

Tuzo na kutambuliwa

  • Tuzo ya Utambuzi kutoka Li TAFO – Kwa mchango katika utetezi wa watu wenye usonji (7 Oktoba 2024)
  • Tuzo ya Umahiri wa Elimu kutoka DICOTA – (27 Septemba 2024)

Machapisho yaliyochaguliwa

  • Predicting the Revisit Interval for Medicare and Medicaid Patients with Type II Diabetes (2019)
  • Frequently Asked Questions About Autism and Their Answers – kwa kushirikiana na Mhandisi Shangwe Mgaya (Novemba 2024)
  • Maswali Yanaoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Usonji na Majibu Yake – tafsiri ya Kiswahili (Novemba 2024)
  • Unveiling Autism: A Journey of Understanding, Advocacy, and Transformation, *The Citizen*, (10 Juni 2024)[2]

Majukwaa na vyombo vya habari

Dr. Lasway ameshiriki katika majukwaa mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, kama vile:

Rejea

  1. "Annie Lasway". Department of Health Administration and Policy. Retrieved 2025-04-23.
  2. "Drama in Nyanza Games as Kisumu Day appeal Agoro Sare loss" [Drama in Nyanza Games as Kisumu Day appeal Agoro Sare loss]. 25 July 2023. Retrieved 2025-04-23.

Jamii:Watu wa Tanzania Jamii:Wanasayansi wa afya Jamii:Wanaharakati wa kijamii Jamii:Wanawake wa Tanzania


This article "Annie Lasway" is from Wikipedia. The list of its authors can be seen in its historical and/or the page Edithistory:Annie Lasway. Articles copied from Draft Namespace on Wikipedia could be seen on the Draft Namespace of Wikipedia and not main one.