RAHMA MAHMOUD
Rahma W. Mahmoud (Mkenga Mbwambo) ni mwandishi wa Vitabu (Riwaya, mashairi, tamthilia), muandaaji wa filamu na muandishi wa habari. Amezaliwa mwaka 1972, Ocean road jijini Dar es Salaam na kukulia katika mtaa wa Libya, Kisutu (uhindini), ulipo katikati ya jiji la Dar es Salaam, nchini Tanzania, Afrika mashariki. Baba yake alikuwa afisa wa posta na simu na mama yake alikuwa mfanyabishara. Ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto sita. Ameolewa na Shuaybu Mahmoud Mruma. Amejaliwa kupata watoto watatu. Kabila la wazazi wake ni Wapare wanatokea Same, mkoani Kilimanjaro. Alipata elimu ya msingi jijini Dar es Salaam, akapata elimu ya sekondari mkoani Kilimanjaro. Alijiunga na chuo cha utumishi wa serikali Magogoni. Baadaye alipata mafunzo mafupi ya uandishi wa habari, uandishi wa vitabu, uchapishaji na haki miliki.
Alisomea mafunzo ya utaalamu wa nguo za wanawake katika chuo cha Sherma na ubunifu wa mitindo mbalimbali ya wanawake na watoto.
Kazi
1. Alikuwa mkurugenzi masoko Thagaji Investment. 2. Alifanya kazi ya uandishi wa habari Business Times, akiandikia gazeti la Majira. 3. Alikuwa mtangazaji wa Radio Times FM, Dar es Salaam Tanzania na muandaaji wa vipindi vya watoto. Mtunzi na mtayarishaji wa simulizi za mila na desturi za kumuandaa msichana katika kabila mbalimbali nchini Tanzania (Mwari wetu), mapishi, utunzi wa riwaya za watu wazima katika kipindi cha Siesta Maisha, kupitia Radio Times. Alikuwa mtangazaji na msimulizi wa sinema za Kihindi katika kipindi cha nyimbo za Kihindi.
Ilikuboresha vipindi vya watoto alipata mafunzo mafupi ya haki za watoto katika kuandaa na kutangaza kupitia shirika la watoto duniani (UNICEF), alishirikiana nalo katika kuandaa siku ya utangazaji wa watoto duniani na siku ya mtoto wa Afrika.
Shughuli nyingine za jamii
1. Alikuwa mjumbe wa kamati ya maandalizi siku ya malaria, Wizara ya Afya. 2. Macmillan Aidan – Tanzania 3. Kuleana Dar es Salaam 4. Kihohede – Dar es Salaam 5. Dogodogo Centre 6. Child in the Sun 7. Ameandika riwaya na mashairi katika magazeti ya Uhuru, Majira, Mwananchi, Dar Leo, Sanifu na Sport Starehe
Uongozi
1. Alikuwa Katibu mkuu wa umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania 2. Alikuwa Katibu mkuu wa umoja wa waandishi wa vitabu wanawake Tanzania (UWAVIWATA). 3. Mjumbe wa kamati kuu ya baraza la vitabu Tanzania (BAMVITA) 1999-2001 4. Mjumbe wa kamati ya wiki ya vitabu Tanzania 1999- 2001.
Uzinduzi wa vitabu Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, kupitia waziri, Mh: Dr. Asharose Migiro walizindua vitabu vyake 14 vya watoto mwaka 2006 katika ukumbi wa Wizara ya Habari na Maelezo, jijini Dar es Salaam.
Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) kupitia mkurugenzi wake Ananilea Nkya waliratibu uzinduzi huo.
Vitabu hivyo vilifadhiliwa na mashirika ya kimataifa ya SIDA, CODE na CIDA. Vinatumika katika maktaba ya shule za msingi Tanzania.
Vitabu hivyo ni
1. Mwindaji kiburi- kisa cha buibui kuishi kwa binadamu 2. Malkia mroho- kisa cha mbwa akimuona chatu humfuata 3. Mateso ya mama wa kambo- Malezi mabaya ya mama wa kambo 4. Kidonda cha bahati- umuhimu wa Elimu kwa Watoto wa kabila la Kimasai na madini yaliyowazunguka. 5. Dawa ya mlafi- athari ya Mtoto kula chakula kupita kiasi 6. Nani kama mama- Mapenzi ya mama kwa mtoto 7. Nangasu mtoto wa mianzini- wazazi wanaozaa na kutupa watoto wachanga. 8. Maua na chipsi dume- Ubakaji na maambukizi ya UKIMWI 9. Mawazo na adha ya usafiri- Matatizo ya usafiri kwa wanafunzi katika miji mikuu. 10. Jiwe la maafa- athari ya mila potofu za mauaji ya watoto wanaoanza kuota meno ya juu 11. Elimu ni ufunguo wa maisha- Athari ya mtoto asiyepata elimu 12. Safari tano za Kadogoo- Umuhimu wa familia kusafiri na tatizo la watoto watundu. 13. Mashaka- kutengwa kwa watoto walemavu kuanzia ngazi ya familia mpaka katika elimu. 14. Mtaji wa masikini- umuhimu wa utunzaji mazingira uanze kutolewa elimu ngazi ya shule.
Baadhi ya vitabu vyake vingine
1. Oldonyolenga 2. Utenzi wa mnazi 3. Bahati 4. Tusome kiushairi kitabu 1-2 5. Tuimbe Alfabeti 6. Mamba asili 7. Binti Afrika na rafiki kutoka China 8. Balozi Tunda-Safari ya bungeni 9. Sauti mafichoni 10. Kisiwa cha kuzimu 11. Mwari wetu 12. Tungo za Rahma binti Shaaban 13. Bustani ya kasri 14. Safari ya Dubai 15. Safari ya Guangzhou China 16. Masikini chungu changu 17. Mizimu imekasirika
Filamu
Kisiwa cha kuzimu- imeonyeshwa katika kituo cha televisheni ya taifa Tanzania (TBC) Mtunzi- Rahma Mahmoud Muongozaji mkuu- Rahma Mahmoud Muongozaji msaidizi- Masiha Muigizaji mkuu – Shamte Kide (S. Kide) Filamu zilizoigizwa bado hazijatoka 1. Filamu - Jambo usilolijua Mtunzi na muongozaji mkuu- Rahma Mahmoud Muigizaji mkuu - Rashid Mtanga Maudhui - Malaria 2. Filamu- Safari ya ndege Mtunzi na Muongozaji mkuu- Rahma Mahmoud Maudhui- Ulemavu si pingamizi katika maisha
Filamu hizi zimetoka katika vitabu vyake na nyingine miswada. Mashindano Rahma amekuwa akiandaa mashindano mbalimbali ya watoto juu ya uwandishi wa vitabu na kutoa zawadi. Aidha amekuwa akifundisha na kuhamasisha jamii hususani wanawake na watoto kuandika vitabu ili kuweza kupata nafasi ya kutoa mawazo yao, hasa ukizingatia ni moja ya jamii iliyopata misukosuko mingi ni wanawake na watoto. Harakati za Wanawake Rahma ameweza kuandaa na kuratibu warsha na semina mbalimbali juu ya uwandishi wa vitabu kwa wanawake Zanzibar, Kilimanjaro na Pwani.
Warsha hizo zilipata ufadhili wa HIVOS.
Harakati za watoto
Amefanikiwa kufundisha watoto juu ya uandishi wa vitabu kati yao wawili alifanikiwa kuwachapisha vitabu.
Aidha amekuwa akiwafundisha watoto juu ya utangazaji na kutoa mawazo na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika siku ya utangazaji ya watoto akishirikiana na Times Radio na UNICEF.
Aliungana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuwapeleka baraza la watoto bungeni mwaka 2005 ili kushinikiza bunge litambue haki zao na maombi yao ikiwemo ya kuruhusiwa kupata nafasi ya uwakilishi bungeni. Shughuli hii ilifadhiliwa na shirika la watoto duniani UNICEF. Utafiti Katika kukuza fani yake ya uandishi wa vitabu alifanya utafiti wa mila na desturi za kumuandaa binti anayetoka katika utoto na kuwa mtu mzima(mwari) kwa makabila mbalimbali nchini Tanzania.
Tafiti hiyo ilijumuisha nyimbo zao, ndoa na historia fupi za wanawake katika harakati za kujiongezea kipato nchini Tanzania.
Mswada huo ulifanyiwa uhariri na mhadhari wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Ujasiriamali
Rahma mjasiriamali mdogo anayefanya biashara zake ndani na nje ya nchi akisafiri China na Dubai.
References
https://books.google.co.tz/books/about/Mwindaji_mwenye_kiburi.html?id=gQ8KAQAAMAAJ&redir_esc=y[1]
This article "RAHMA MAHMOUD" is from Wikipedia. The list of its authors can be seen in its historical and/or the page Edithistory:RAHMA MAHMOUD. Articles copied from Draft Namespace on Wikipedia could be seen on the Draft Namespace of Wikipedia and not main one.
